Pular para o conteúdo
Publicidade

Kutoka 4:1-5

SRUV Swahili Revised Union Version

Musa afanya miujiza

1 Musa akajibu akasema, Lakini, tazama, hawataniamini, wala hawataisikia sauti yangu; maana watasema, BWANA hakukutokea. 2 BWANA akamwambia, Ni nini hiyo uliyo nayo mkononi mwako? Akasema, Ni fimbo. 3 Akamwambia, Itupe chini; akaitupa chini, nayo ikawa nyoka; Musa akakimbia kutoka mbele yake. 4 BWANA akamwambia Musa, Nyosha mkono wako, kamshike mkia; (akaunyosha mkono wake akamshika, naye akageuka kuwa fimbo mkononi mwake;) 5 Kut 19:9ili kwamba wapate kusadiki ya kwamba BWANA, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amekutokea.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    1 Musa akamjibu, "Itakuwaje wasiponiamini au kunisikiliza, waseme, ‘Mwenyezi Mungu hakukutokea’?"

    2 Ndipo Mwenyezi Mungu akamuuliza, "Ni nini hicho kilicho mkononi mwako?"

    Akamjibu, "Ni fimbo."

    3 Mwenyezi Mungu akasema, "Itupe chini."

    Musa akaitupa fimbo chini, nayo ikawa nyoka, naye akaikimbia. 4 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia, "Nyoosha mkono wako umkamate kwenye mkia." Basi Musa akanyoosha mkono akamkamata yule nyoka, naye akabadilika tena kuwa fimbo mkononi mwake. 5 Mwenyezi Mungu akasema, "Hivi ndivyo Waisraeli watakavyoamini kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo, amekutokea wewe."

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    1 Mose akamjibu, "Itakuwaje kama hawataniamini au kunisikiliza, waseme, ‘Bwana hakukutokea’?"

    2 Ndipo Bwana akamwambia, "Ni nini hicho kilicho mkononi mwako?"

    Akajibu, "Fimbo."

    3 Bwana akasema, "Itupe chini."

    Mose akaitupa chini hiyo fimbo nayo ikawa nyoka, naye akaikimbia. 4 Kisha Bwana akamwambia, "Nyoosha mkono wako umkamate mkiani." Basi Mose akanyoosha mkono akamkamata yule nyoka, naye akabadilika tena kuwa fimbo mkononi mwake. 5 Bwana akasema, "Hivi ndivyo Waisraeli watakavyoamini kuwa Bwana, Mungu wa baba zao, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaki, na Mungu wa Yakobo, amekutokea wewe."

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.