27 Kwa maana imeandikwa:
"Furahi, ewe mwanamke tasa,
wewe usiyezaa;
paza sauti, na kuimba kwa furaha,
wewe usiyepatwa na utungu wa kuzaa;
kwa maana watoto wa mwanamke aliyeachwa ukiwa ni wengi
kuliko wa mwanamke mwenye mume."
28 Basi, sisi ndugu zangu, ni kama Isaki, tu watoto wa ahadi. 29 Lakini, kama vile ilivyokuwa siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomchokoza yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo hata sasa.