27 Kwa maana imeandikwa:
"Furahi, ewe mwanamke tasa,
wewe usiyezaa;
paza sauti, na kuimba kwa furaha,
wewe usiyepatwa na uchungu wa kuzaa;
kwa maana watoto wa mwanamke aliyeachwa ukiwa ni wengi
kuliko wa mwanamke mwenye mume."
28 Basi, sisi ndugu zangu, ni kama Isaka, tu watoto wa ahadi. 29 Lakini, kama vile ilivyokuwa siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomchokoza yule aliyezaliwa kwa uweza wa Roho wa Mungu, ndivyo ilivyo hata sasa.