Pular para o conteúdo
Publicidade

Mwanzo 3:7-10,21

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

7 Ndipo macho yao wote wawili yakafumbuliwa, wakajiona kwamba walikuwa uchi; hivyo wakashona majani ya mtini, wakajifunika.

8 Ndipo yule mwanaume na mkewe, waliposikia sauti ya Bwana Mungu alipokuwa akitembea bustanini jioni, wakajificha kutoka mbele za Bwana Mungu katikati ya miti ya bustani. 9 Lakini Bwana Mungu akamwita Adamu, "Uko wapi?"

10 Naye akajibu, "Nilikusikia katika bustani nikaogopa kwa sababu nilikuwa uchi, hivyo nikajificha."

21 Bwana Mungu akawatengenezea Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    7 Ndipo macho yao wote wawili yakafumbuliwa, wakajiona kwamba walikuwa uchi; hivyo wakashona majani ya mtini, wakajifunika.

    8 Yule mwanaume na mkewe waliposikia sauti ya Bwana Mwenyezi Mungu akitembea bustanini jioni, wakajificha kutoka kwa Bwana Mwenyezi Mungu katikati ya miti ya bustani. 9 Lakini Bwana Mwenyezi Mungu akamwita Adamu, "Uko wapi?"

    10 Naye akajibu, "Nilikusikia katika bustani nikaogopa kwa sababu nilikuwa uchi, hivyo nikajificha."

    21 Bwana Mwenyezi Mungu akawatengenezea Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    7 Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajitambua kuwa wako uchi, wakashona majani ya mtini, na kujifanyia mavazi ya kusitiri uchi wao. 8 Ayu 31:33;38:1;Zab 139:1-12;Yer 23:34;Amo 9:3Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone. 9 Mwa 4:9BWANA Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? 10 Ayu 23:15;1 Yoh 3:20Akasema, Nilisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.

    21 BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.