7 Ndipo macho yao wote wawili yakafumbuliwa, wakajiona kwamba walikuwa uchi; hivyo wakashona majani ya mtini, wakajifunika.
8 Yule mwanaume na mkewe waliposikia sauti ya Bwana Mwenyezi Mungu akitembea bustanini jioni, wakajificha kutoka kwa Bwana Mwenyezi Mungu katikati ya miti ya bustani. 9 Lakini Bwana Mwenyezi Mungu akamwita Adamu, "Uko wapi?"
10 Naye akajibu, "Nilikusikia katika bustani nikaogopa kwa sababu nilikuwa uchi, hivyo nikajificha."
21 Bwana Mwenyezi Mungu akawatengenezea Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.