7 Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajitambua kuwa wako uchi, wakashona majani ya mtini, na kujifanyia mavazi ya kusitiri uchi wao. 8 Ayu 31:33;38:1;Zab 139:1-12;Yer 23:34;Amo 9:3Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone. 9 Mwa 4:9BWANA Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? 10 Ayu 23:15;1 Yoh 3:20Akasema, Nilisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.
21 BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.