5 Yosefu akaota ndoto, naye alipowaeleza ndugu zake, wakamchukia zaidi. 6 Akawaambia, "Sikilizeni ndoto niliyoota: 7 Tulikuwa tukifunga miganda ya nafaka shambani, ghafula mganda wangu ukasimama wima, wakati miganda yenu ikiuzunguka na kuuinamia."
8 Ndugu zake wakamwambia, "Wewe unakusudia kututawala? Hivi kweli wewe utatutawala sisi?" Wakaongeza kumchukia zaidi kwa sababu ya ndoto yake pamoja na yale aliyowaambia.
9 Kisha akaota ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake akisema, "Sikilizeni, nimeota ndoto nyingine, wakati huu jua, mwezi na nyota kumi na moja zilikuwa zinanisujudia."