5 Yusufu akaota ndoto, naye alipowaeleza ndugu zake, wakamchukia zaidi. 6 Akawaambia, "Sikilizeni ndoto niliyoota: 7 Tulikuwa tukifunga miganda ya nafaka shambani. Ghafula mganda wangu ukasimama wima, nayo miganda yenu ikauzunguka na kuuinamia."
8 Ndugu zake wakamwambia, "Wewe unakusudia kututawala? Hivi kweli wewe utatutawala sisi?" Wakazidi kumchukia kwa sababu ya ndoto yake, pamoja na yale aliyowaambia.
9 Kisha akaota ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake, akisema, "Sikilizeni: nimeota ndoto nyingine. Wakati huu jua, mwezi na nyota kumi na moja zilikuwa zinanisujudia."