Pular para o conteúdo
Publicidade

Mwanzo 37:5-9

SRUV Swahili Revised Union Version

5 Yusufu akaota ndoto, akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi kumchukia; 6 akawaambia, Tafadhalini, sikieni ndoto hii niliyoiota. 7 Mwa 42:6;43:26;44:14Tazama, sisi tulikuwa tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama, miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu. 8 Ndugu zake wakamwambia, Je! Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? Wakazidi kumchukia kwa ajili ya ndoto yake, na kwa maneno yake.

9 Mwa 46:29Akaota tena ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake, akasema, Angalieni, nimeota ndoto nyingine; na tazama, jua na mwezi na nyota kumi na moja zikaniinamia.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    5 Yusufu akaota ndoto, naye alipowaeleza ndugu zake, wakamchukia zaidi. 6 Akawaambia, "Sikilizeni ndoto niliyoota: 7 Tulikuwa tukifunga miganda ya nafaka shambani. Ghafula mganda wangu ukasimama wima, nayo miganda yenu ikauzunguka na kuuinamia."

    8 Ndugu zake wakamwambia, "Wewe unakusudia kututawala? Hivi kweli wewe utatutawala sisi?" Wakazidi kumchukia kwa sababu ya ndoto yake, pamoja na yale aliyowaambia.

    9 Kisha akaota ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake, akisema, "Sikilizeni: nimeota ndoto nyingine. Wakati huu jua, mwezi na nyota kumi na moja zilikuwa zinanisujudia."

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    5 Yosefu akaota ndoto, naye alipowaeleza ndugu zake, wakamchukia zaidi. 6 Akawaambia, "Sikilizeni ndoto niliyoota: 7 Tulikuwa tukifunga miganda ya nafaka shambani, ghafula mganda wangu ukasimama wima, wakati miganda yenu ikiuzunguka na kuuinamia."

    8 Ndugu zake wakamwambia, "Wewe unakusudia kututawala? Hivi kweli wewe utatutawala sisi?" Wakaongeza kumchukia zaidi kwa sababu ya ndoto yake pamoja na yale aliyowaambia.

    9 Kisha akaota ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake akisema, "Sikilizeni, nimeota ndoto nyingine, wakati huu jua, mwezi na nyota kumi na moja zilikuwa zinanisujudia."

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.