8 Wakamjibu, "Sisi sote tuliota ndoto, lakini hapakuwa na mtu yeyote wa kuzifasiri."
Ndipo Yosefu akawaambia, "Je, kufasiri ndoto si kazi ya Mungu? Niambieni ndoto zenu."
12 Yosefu akamwambia, "Hii ndiyo maana yake: Matawi matatu ni siku tatu. 13 Katika siku hizi tatu, Farao atakutoa gerezani na kukuweka tena kwenye nafasi yako, nawe utaweka kikombe cha Farao mikononi mwake, kama vile ulivyokuwa unafanya ulipokuwa mnyweshaji wake.
18 Yosefu akamwambia, "Hii ndiyo maana yake: Vikapu vitatu ni siku tatu. 19 Katika siku hizi tatu, Farao atakata kichwa chako na kukutundika juu ya mti. Nao ndege watakula nyama ya mwili wako."