8 Wakamjibu, "Sisi sote tumeota ndoto, lakini hakuna wa kuzifasiri."
Ndipo Yusufu akawaambia, "Je, kufasiri ndoto si ni kazi ya Mungu? Niambieni ndoto zenu."
12 Yusufu akamwambia, "Hii ndiyo maana yake: Matawi matatu ni siku tatu. 13 Baada ya siku tatu, Farao atakutoa gerezani na kukurudisha kwenye nafasi yako, nawe utaweka kikombe cha Farao mkononi mwake, jinsi ulivyofanya ulipokuwa mnyweshaji wake awali.
18 Yusufu akamwambia, "Hii ndiyo maana yake: Vikapu vitatu ni siku tatu. 19 Baada ya siku tatu, Farao atakata kichwa chako na kukutundika juu ya mti. Nao ndege watakula nyama ya mwili wako."