Pular para o conteúdo
Publicidade

Mwanzo 40:8,12,13,18,19

SRUV Swahili Revised Union Version

8 Mwa 41:15,16;Dan 2:11Wakamwambia, Tumeota ndoto wala hapana awezaye kuifasiri. Yusufu akawaambia, Nawaomba mniambie, kufasiri si ni kazi ya Mungu? 12 Amu 7:14;Dan 2:36;4:19Yusufu akamwambia, Tafsiri yake ndiyo hii. Matawi matatu ni siku tatu. 13 Zab 3:3;Yer 52:31Baada ya siku tatu Farao atakiinua kichwa chako, atakurudisha katika kazi yako; nawe utampa Farao kikombe mkononi mwake, kama desturi ya kwanza, ulipokuwa mnyweshaji wake.

18 Yusufu akajibu, akasema, Tafsiri yake ndiyo hii Nyungo tatu ni siku tatu. 19 Baada ya siku tatu Farao atakiinua na kukuondolea kichwa chako, na kukutundika juu ya mti, na ndege watakula nyama yako.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    8 Wakamjibu, "Sisi sote tumeota ndoto, lakini hakuna wa kuzifasiri."

    Ndipo Yusufu akawaambia, "Je, kufasiri ndoto si ni kazi ya Mungu? Niambieni ndoto zenu."

    12 Yusufu akamwambia, "Hii ndiyo maana yake: Matawi matatu ni siku tatu. 13 Baada ya siku tatu, Farao atakutoa gerezani na kukurudisha kwenye nafasi yako, nawe utaweka kikombe cha Farao mkononi mwake, jinsi ulivyofanya ulipokuwa mnyweshaji wake awali.

    18 Yusufu akamwambia, "Hii ndiyo maana yake: Vikapu vitatu ni siku tatu. 19 Baada ya siku tatu, Farao atakata kichwa chako na kukutundika juu ya mti. Nao ndege watakula nyama ya mwili wako."

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    8 Wakamjibu, "Sisi sote tuliota ndoto, lakini hapakuwa na mtu yeyote wa kuzifasiri."

    Ndipo Yosefu akawaambia, "Je, kufasiri ndoto si kazi ya Mungu? Niambieni ndoto zenu."

    12 Yosefu akamwambia, "Hii ndiyo maana yake: Matawi matatu ni siku tatu. 13 Katika siku hizi tatu, Farao atakutoa gerezani na kukuweka tena kwenye nafasi yako, nawe utaweka kikombe cha Farao mikononi mwake, kama vile ulivyokuwa unafanya ulipokuwa mnyweshaji wake.

    18 Yosefu akamwambia, "Hii ndiyo maana yake: Vikapu vitatu ni siku tatu. 19 Katika siku hizi tatu, Farao atakata kichwa chako na kukutundika juu ya mti. Nao ndege watakula nyama ya mwili wako."

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.