Pular para o conteúdo
Publicidade

Isaya 12

Kushukuru Na Kusifu

1 Katika siku ile utasema:

"Nitakusifu wewe, Ee Bwana.

Ingawa ulinikasirikia,

hasira yako imegeukia mbali

nawe umenifariji.

2 Hakika Mungu ni wokovu wangu;

nitamtumaini wala sitaogopa.

Bwana, Bwana, ni nguvu zangu na wimbo wangu;

amekuwa wokovu wangu."

3 Kwa furaha mtachota maji

kutoka visima vya wokovu.

4 Katika siku hiyo mtasema:

"Mshukuruni Bwana, mliitie jina lake;

julisheni miongoni mwa mataifa yale aliyoyafanya,

tangazeni kuwa jina lake limetukuka.

5 Mwimbieni Bwana, kwa kuwa ametenda mambo makuu,

hili na lijulikane duniani kote.

6 Pazeni sauti mwimbe kwa furaha, watu wa Sayuni,

kwa maana mkuu ni yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli miongoni mwenu."

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também