Pular para o conteúdo
Publicidade

Isaya 40:27-31

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

27 Kwa nini unasema, ee Yakobo,

nanyi ee Israeli, kulalamika,

"Njia yangu imefichwa Bwana asiione,

Mungu wangu hajali shauri langu?"

28 Je wewe, hufahamu?

Je wewe, hujasikia?

Bwana ni Mungu wa milele,

Muumba wa miisho ya dunia.

Hatachoka wala kulegea,

wala hakuna hata mmoja

awezaye kuupima ufahamu wake.

29 Huwapa nguvu waliolegea

na huongeza nguvu za wadhaifu.

30 Hata vijana huchoka na kulegea,

nao vijana wanaume hujikwaa na kuanguka,

31 bali wale wamtumainio Bwana

atafanya upya nguvu zao.

Watapaa juu kwa mbawa kama tai;

watapiga mbio wala hawatachoka,

watatembea kwa miguu wala hawatazimia.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    27 Kwa nini unasema, ee Yakobo,

    nanyi ee Israeli, kulalamika,

    "Njia yangu imefichwa Mwenyezi Mungu asiione,

    Mungu wangu hajali shauri langu?"

    28 Je wewe, hufahamu?

    Je wewe, hujasikia?

    Mwenyezi Mungu ni Mungu wa milele,

    Muumba wa miisho ya dunia.

    Hatachoka wala kulegea,

    wala hakuna hata mmoja

    awezaye kuupima ufahamu wake.

    29 Huwapa nguvu waliolegea

    na huongeza nguvu za wadhaifu.

    30 Hata vijana huchoka na kulegea,

    nao vijana wanaume hujikwaa na kuanguka,

    31 bali wale wamtumainio Mwenyezi Mungu

    atafanya upya nguvu zao.

    Watapaa juu kwa mabawa kama tai;

    watapiga mbio wala hawatachoka,

    watatembea kwa miguu wala hawatazimia.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    27 Mbona unasema, Ee Yakobo, mbona unanena, Ee Israeli, Njia yangu imefichwa, BWANA asiione, na hukumu yangu imempita Mungu wangu asiiangalie? 28 Zab 147:5;Rum 11:33Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki. 29 Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo. 30 Hata vijana watazimia na kuchoka, na vijana wanaume wataanguka; 31 Ayu 17:9;Zab 25:3;Isa 8:17;Omb 3:25;2 Kor 4:8-10,16bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watakimbia, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.