Pular para o conteúdo
Publicidade

Isaya 58:3-7

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

3 Wao husema, ‘Mbona tumefunga, nawe hujaona?

Mbona tumejinyenyekeza, nawe huangalii?’

"Lakini katika siku ya kufunga kwenu, mnafanya mnavyotaka

na kuwadhulumu wafanyakazi wenu wote.

4 Kufunga kwenu huishia kwenye magomvi na mapigano,

na kupigana ninyi kwa ninyi kwa ngumi za uovu.

Hamwezi kufunga kama mnavyofanya leo

na kutazamia sauti zenu kusikiwa huko juu.

5 Je, hii ndiyo aina ya mfungo niliouchagua,

siku moja tu ya mtu kujinyenyekeza?

Je, ni kwa kuinamisha kichwa chini kama tete,

na kwa kujilaza juu ya nguo ya gunia na majivu?

Je, huo ndio mnaouita mfungo,

siku iliyokubalika kwa Bwana?

6 "Je, hii si ndiyo aina ya mfungo niliyoichagua:

kufungua minyororo ya udhalimu,

na kufungua kamba za nira,

kuwaweka huru walioonewa,

na kuvunja kila nira?

7 Je, sio kushirikiana chakula chako na wenye njaa

na kuwapatia maskini wasiokuwa na makao hifadhi,

unapomwona aliye uchi, umvike,

wala si kumkimbia mtu wa nyama na damu yako mwenyewe?

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    3 Wao husema, ‘Mbona tumefunga, nawe hujaona?

    Mbona tumejinyenyekeza, nawe huangalii?’

    "Lakini katika siku ya kufunga kwenu, mnafanya mnavyotaka

    na kuwadhulumu wafanyakazi wenu wote.

    4 Kufunga kwenu huishia kwenye magomvi na mapigano,

    na kupigana ninyi kwa ninyi kwa ngumi za uovu.

    Hamwezi kufunga kama mnavyofanya leo

    na kutazamia sauti zenu kusikiwa huko juu.

    5 Je, hii ndiyo aina ya mfungo niliouchagua,

    siku moja tu ya mtu kujinyenyekeza?

    Je, ni kwa kuinamisha kichwa chini kama tete,

    na kwa kujilaza juu ya gunia na majivu?

    Je, huo ndio mnaouita mfungo,

    siku iliyokubalika kwa Mwenyezi Mungu?

    6 "Je, hii si ndiyo aina ya mfungo niliyoichagua:

    kufungua minyororo ya udhalimu,

    na kufungua kamba za nira,

    kuwaweka huru waliodhulumiwa,

    na kuvunja kila nira?

    7 Je, sio kushirikiana chakula chako na wenye njaa

    na kuwapatia maskini wasiokuwa na makao hifadhi,

    unapomwona aliye uchi, umvike,

    wala si kumkimbia mtu wa mwili wako

    na damu yako mwenyewe?

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    3 Mal 3:14Husema, Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini huangalii? Fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu. 4 Tazama, ninyi mnafunga ili mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwa ngumi ya uovu. Kufunga kama huku kwa siku ya leo hakutafanya sauti zenu zisikike juu. 5 Zek 7:5Je! Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na BWANA? 6 Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira? 7 Mt 25:34;Zab 112:9;Mit 22:9;Mhu 11:1,2;Dan 4:27;Lk 11:41;Mwa 29:14;Neh 5:5;Mt 15:5Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usikose kumsaidia mtu aliye jamaa yako.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.