9 Ninawaombea wao. Mimi siuombei ulimwengu, bali nawaombea wale ulionipa kwa sababu wao ni wako. 11 Mimi sasa simo tena ulimwenguni, lakini wao bado wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba Mtakatifu, uwalinde kwa uweza wa jina lako ulilonipa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo wamoja.
15 Siombi kwamba uwaondoe ulimwenguni, bali uwalinde dhidi ya yule mwovu.
Yesu Awaombea Wote Wamwaminio
20 "Siwaombei hawa peke yao, bali nawaombea na wale wote watakaoniamini kupitia neno lao