Pular para o conteúdo
Publicidade

Yeremia 28:1-3,15-17

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

Hanania Nabii Wa Uongo

1 Katika mwezi wa tano wa mwaka ule ule, yaani mwaka wa nne, mwanzoni mwa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, nabii Hanania mwana wa Azuri, ambaye alitoka Gibeoni, akaniambia katika nyumba ya Bwana mbele ya makuhani na watu wote: 2 "Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli asemalo: ‘Nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli. 3 Katika muda wa miaka miwili nitavirudisha mahali hapa vyombo vyote vya nyumba ya Bwana ambavyo Nebukadneza mfalme wa Babeli aliviondoa kutoka hapa na kuvipeleka Babeli.

15 Kisha nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, "Sikiliza Hanania! Bwana hajakutuma, lakini wewe umelishawishi taifa hili kuamini uongo. 16 Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Bwana: ‘Hivi karibuni nitakuondoa kutoka juu ya uso wa dunia. Mwaka huu utakufa, kwa sababu umetangaza uasi dhidi ya Bwana.’ "

17 Katika mwezi wa saba wa mwaka ule ule, nabii Hanania akafa.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    1 Katika mwezi wa tano wa mwaka ule ule, yaani mwaka wa nne, mwanzoni mwa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, nabii Hanania mwana wa Azuri, ambaye alitoka Gibeoni, akaniambia katika nyumba ya Mwenyezi Mungu mbele ya makuhani na watu wote: 2 "Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli asemalo: ‘Nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli. 3 Katika muda wa miaka miwili nitavirudisha mahali hapa vyombo vyote vya nyumba ya Mwenyezi Mungu ambavyo Nebukadneza mfalme wa Babeli aliviondoa kutoka hapa na kuvipeleka Babeli.

    15 Kisha nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, "Sikiliza Hanania! Mwenyezi Mungu hajakutuma, lakini wewe umelishawishi taifa hili kuamini uongo. 16 Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Hivi karibuni nitakuondoa duniani. Mwaka huu utakufa, kwa sababu umetangaza uasi dhidi ya Mwenyezi Mungu.’ "

    17 Katika mwezi wa saba wa mwaka ule ule, nabii Hanania akafa.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    1 Yer 27:1;36:12;2 Tim 2:8;2 Pet 2:1;2 Fal 24:18-20;2 Nya 36:11-13Ikawa, katika mwaka ule ule, mwanzo wa kutawala kwake Sedekia, mfalme wa Yuda, mwaka wa nne, mwezi wa tano, Hanania, mwana wa Azuri, nabii, wa Gibeoni, akasema nami ndani ya nyumba ya BWANA, mbele ya makuhani na watu wote, akisema, 2 Yer 27:12BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nimeivunja nira ya mfalme wa Babeli. 3 2 Fal 24:13;2 Nya 36:10;Yer 27:16-22Kabla haujatimia muda wa miaka miwili mizima, nitavirudisha mahali hapa vyombo vyote vya nyumba ya BWANA, ambavyo Nebukadneza, mfalme wa Babeli, aliviondoa kutoka mahali hapa, akavipeleka mpaka Babeli.

    15 Yer 20:6;29:31Kisha nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, Sikia sasa, Ee Hanania; BWANA hakukutuma; lakini unawapa tumaini watu hawa kwa maneno ya uongo. 16 Basi BWANA asema hivi, Tazama, nakutuma uende zako toka juu ya uso wa nchi; mwaka huu utakufa, kwa sababu umenena maneno ya uasi juu ya BWANA. 17 Basi nabii Hanania akafa, mwaka uo huo, mwezi wa saba.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.