Hanania nabii wa uongo
1 Katika mwezi wa tano wa mwaka ule ule, yaani mwaka wa nne, mwanzoni mwa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, nabii Hanania mwana wa Azuri, ambaye alitoka Gibeoni, akaniambia katika nyumba ya Mwenyezi Mungu mbele ya makuhani na watu wote: 2 "Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli asemalo: ‘Nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli. 3 Katika muda wa miaka miwili nitavirudisha mahali hapa vyombo vyote vya nyumba ya Mwenyezi Mungu ambavyo Nebukadneza mfalme wa Babeli aliviondoa kutoka hapa na kuvipeleka Babeli.
15 Kisha nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, "Sikiliza Hanania! Mwenyezi Mungu hajakutuma, lakini wewe umelishawishi taifa hili kuamini uongo. 16 Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Hivi karibuni nitakuondoa duniani. Mwaka huu utakufa, kwa sababu umetangaza uasi dhidi ya Mwenyezi Mungu.’ "
17 Katika mwezi wa saba wa mwaka ule ule, nabii Hanania akafa.