Pular para o conteúdo
Publicidade

Yeremia 29:11-14

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

11 Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu," asema Bwana, "ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo. 12 Kisha mtaniita, na mtakuja na kuniomba, nami nitawasikiliza. 13 Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. 14 Nitaonekana kwenu," asema Bwana, "nami nitawarudisha watu wenu waliotekwa. Nitawakusanya kutoka mataifa yote na mahali pote nilipokuwa nimewafukuzia, nami nitawarudisha mahali ambapo nilikuwa nimewatoa walipochukuliwa uhamishoni," asema Bwana.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    11 Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu," asema Mwenyezi Mungu, "ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo. 12 Kisha mtaniita, na mtakuja na kuniomba, nami nitawasikiliza. 13 Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wote. 14 Nitaonekana kwenu," asema Mwenyezi Mungu, "nami nitawarudisha watu wenu waliotekwa. Nitawakusanya kutoka mataifa yote na mahali pote nilipokuwa nimewafukuzia, nami nitawarudisha mahali nilipokuwa nimewatoa walipopelekwa uhamishoni," asema Mwenyezi Mungu.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za baadaye. 12 Dan 9:3Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza. 13 Law 26:39,40;Zab 32:6;Mt 7:7;Yer 24:7;Kum 4:29Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. 14 Kum 4:7;Zab 32:6;Isa 55:6;Rum 10:20;Yer 23:3,8;30:3Nami nitaonekana kwenu, asema BWANA, nami nitawarudisha watu wenu waliofungwa, nami nitawakusanya ninyi, nikiwatoa katika mataifa yote, na katika mahali pote, nilikowafukuza, asema BWANA; nami nitawaleta tena, hadi mahali ambapo kutoka hapo niliwafanya mchukuliwe mateka.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.