11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za baadaye. 12 Dan 9:3Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza. 13 Law 26:39,40;Zab 32:6;Mt 7:7;Yer 24:7;Kum 4:29Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. 14 Kum 4:7;Zab 32:6;Isa 55:6;Rum 10:20;Yer 23:3,8;30:3Nami nitaonekana kwenu, asema BWANA, nami nitawarudisha watu wenu waliofungwa, nami nitawakusanya ninyi, nikiwatoa katika mataifa yote, na katika mahali pote, nilikowafukuza, asema BWANA; nami nitawaleta tena, hadi mahali ambapo kutoka hapo niliwafanya mchukuliwe mateka.
Publicidade