Pular para o conteúdo
Publicidade

Yeremia 47

Hukumu juu ya Wafilisti

1 Sef 2:4-7;Zek 9:5-7 Neno la BWANA lililomjia Yeremia, nabii, kuhusu Wafilisti, kabla Farao hajashambulia Gaza. Isa 14:29-31;Eze 25:15-17;Yoe 3:4-8;Amo 1:6-8;Sef 2:4-7;Zek 9:5-7

2 Isa 8:7;Yer 1:14 BWANA asema hivi, Tazama, maji yanatokea katika pande za kaskazini, nayo yatakuwa mto ufurikao, nayo yataifunika nchi, na kila kitu kilichomo, huo mji na wote wakaao ndani yake; nao watu watalia na watu wote wakaao katika nchi wataomboleza. 3 Nah 3:2 Kwa sababu ya kishindo cha kukanyaga kwa kwato za farasi wake walio hodari, kwa sababu ya mwendo wa mbio mbio wa magari yake ya vita; kwa sababu ya mngurumo wa magurudumu yake, hao akina baba hawatazami nyuma ili kuwaangalia watoto wao, kwa kuwa mikono yao ni dhaifu; 4 Yer 25:22;Yoe 3:4;Amo 1:9,10;9:7;Mwa 10:14 kwa sababu ya siku ijayo kuwaangamiza Wafilisti wote, kukatilia mbali kila msaidizi wa Tiro na Sidoni asaliaye; maana BWANA atawaharibu Wafilisti, mabaki ya kisiwa cha Kaftori.

5 Sef 2:4 Upaa umeupata Gaza;

Ashkeloni umenyamazishwa

Mabaki ya bonde lao;

Hata lini utajikatakata?

6 Eze 21:3 Ee upanga wa BWANA,

Siku ngapi zitapita kabla hujatulia?

Ujitie katika ala yako;

Pumzika, utulie.

7 1 Sam 3:12;Mik 6:9 Utawezaje kutulia,

Ikiwa BWANA amekupa agizo?

Juu ya Ashkeloni na juu ya pwani,

Ndipo alipoyaamuru hayo.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também