Pular para o conteúdo
Publicidade

Yoshua 24:14-16,23,24

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

14 "Sasa basi mcheni Bwana na kumtumikia kwa uaminifu wote. Itupeni mbali miungu ambayo baba zenu waliiabudu huko ngʼambo ya Mto Frati na huko Misri, nanyi mtumikieni Bwana. 15 Lakini msipoona vyema kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia, kama ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ngʼambo Frati, au miungu ya Waamori, ambao mnakaa katika nchi yao. Lakini mimi na nyumba yangu, tutamtumikia Bwana."

16 Ndipo hao watu wakajibu, "Hili jambo liwe mbali nasi la kumsahau Bwana na kuitumikia miungu mingine!

23 Yoshua akawaambia, "Sasa basi, itupeni mbali hiyo miungu migeni iliyo katikati yenu, nanyi mtoleeni Bwana, Mungu wa Israeli, mioyo yenu."

24 Nao watu wakamwambia Yoshua, "Tutamtumikia Bwana Mungu wetu na kumtii yeye."

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    14 "Sasa basi mcheni Mwenyezi Mungu na kumtumikia kwa uaminifu wote. Itupeni mbali miungu ambayo baba zenu waliiabudu huko ng’ambo ya Mto na huko Misri, nanyi mtumikieni Mwenyezi Mungu. 15 Lakini msipoona vyema kumtumikia Mwenyezi Mungu, chagueni hivi leo mtakayemtumikia, kama ni miungu ile baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Frati, au miungu ya Waamori, ambao mnakaa katika nchi yao. Lakini mimi na nyumba yangu, tutamtumikia Mwenyezi Mungu."

    16 Ndipo hao watu wakajibu, "Hili jambo liwe mbali nasi la kumsahau Mwenyezi Mungu na kuitumikia miungu mingine!

    23 Yoshua akawaambia, "Sasa basi, itupeni mbali hiyo miungu migeni mliyo nayo, nanyi mtoleeni Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, mioyo yenu."

    24 Nao watu wakamwambia Yoshua, "Tutamtumikia Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, na kumtii yeye."

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    14 Kum 10:12;1 Sam 12:24;Ayu 1:1;Mdo 9:31;Mwa 17:1;20:5;Kum 18:13;Zab 119:1;2 Kor 1:12;Efe 6:24;Law 17:7;Eze 20:7Basi sasa mcheni BWANA, mkamtumikie kwa unyofu wa moyo na kwa kweli; na kuiweka mbali miungu ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, na huko Misri; mkamtumikie yeye BWANA. 15 Kut 23:24;Kum 13:7;Amu 6:10;Mwa 18:19Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA. 16 Hao watu wakajibu wakasema, Hasha! Tusimwache BWANA, ili kuitumikia miungu mingine; 23 Mwa 35:2;1 Sam 7:3Akasema, Basi sasa, iondoeni miungu migeni iliyo kati yenu, mkaielekeze mioyo yenu kwa BWANA, Mungu wa Israeli. 24 Ndipo hao watu wakamwambia Yoshua, BWANA, Mungu wetu, ndiye tutakayemtumikia; na sauti yake ndiyo tutakayoitii.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.