14 "Sasa basi mcheni Mwenyezi Mungu na kumtumikia kwa uaminifu wote. Itupeni mbali miungu ambayo baba zenu waliiabudu huko ng’ambo ya Mto na huko Misri, nanyi mtumikieni Mwenyezi Mungu. 15 Lakini msipoona vyema kumtumikia Mwenyezi Mungu, chagueni hivi leo mtakayemtumikia, kama ni miungu ile baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Frati, au miungu ya Waamori, ambao mnakaa katika nchi yao. Lakini mimi na nyumba yangu, tutamtumikia Mwenyezi Mungu."
16 Ndipo hao watu wakajibu, "Hili jambo liwe mbali nasi la kumsahau Mwenyezi Mungu na kuitumikia miungu mingine!
23 Yoshua akawaambia, "Sasa basi, itupeni mbali hiyo miungu migeni mliyo nayo, nanyi mtoleeni Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, mioyo yenu."
24 Nao watu wakamwambia Yoshua, "Tutamtumikia Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, na kumtii yeye."