20 Yule mwanamke akamwita, "Samsoni, hao Wafilisti wanakujia!"
Akaamka toka usingizini akasema, "Nitatoka nje kama hapo awali, nitawakungʼutia mbali na kuwa huru." Lakini hakujua kuwa Bwana amemwacha.
22 Wakati huo nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa.
28 Ndipo Samsoni akamwomba Bwana, akasema, "Ee Bwana Mwenyezi, unikumbuke. Ee Mungu, nakusihi ukanitie nguvu mara hii moja tena, ili kwa tendo hili nipate kulipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili."