20 Yule mwanamke akamwita, "Samsoni! Hao, Wafilisti wanakujia!"
Akaamka toka usingizini, akisema, "Nitatoka nje kama hapo awali; nitajinyoosha, niwe huru." Lakini hakujua kwamba Mwenyezi Mungu alikuwa amemwacha.
22 Wakati huo nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa.
28 Ndipo Samsoni akamwomba Mwenyezi Mungu, akasema, "Ee Bwana Mungu Mwenyezi, unikumbuke. Ee Mungu, nakusihi ukanitie nguvu mara hii moja tu, ili kwa tendo hili nipate kulipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa sababu ya macho yangu mawili."