11 Malaika wa Bwana akaja akaketi chini ya mti wa mwaloni huko Ofra, ambao ulikuwa mali ya Yoashi, Mwabiezeri, ambako Gideoni mwanawe alikuwa akipepeta ngano penye shinikizo la kukamulia zabibu, ili kuificha Wamidiani wasiione. 12 Malaika wa Bwana alipomtokea Gideoni, akamwambia, "Bwana yu pamoja nawe, Ewe shujaa mwenye nguvu."
22 Gideoni alipotambua kuwa ni malaika wa Bwana, akapiga kelele kwa mshangao, akasema, "Ole wangu, Bwana Mwenyezi! Kwa kuwa nimemwona malaika wa Bwana uso kwa uso!"
23 Lakini Bwana akamwambia, "Amani iwe kwako! Usiogope. Hutakufa."
24 Hivyo Gideoni akamjengea Bwana madhabahu mahali pale na kupaita, Yehova-Shalom.6:24 Yehova-Shalom maana yake Bwana ni Amani. Mpaka leo ingalipo imesimama huko Ofra ya Waabiezeri.