Gideoni aitwa na Mungu
11 Yos 17:2;Amu 8:2Malaika wa BWANA akaenda akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika Ofra, uliokuwa mali yake Yoashi, Mwaabiezeri; na mwanawe Gideoni alikuwa akipepeta ngano ndani ya shinikizo, ili kuificha machoni pa Wamidiani. 12 Mwa 16:7-13;Amu 13:3;Lk 1:11,28Malaika wa BWANA akamtokea, akamwambia, BWANA yuko pamoja nawe, Ee shujaa.
22 Mwa 16:13;32:30;Kut 33:20;Amu 13:22Gideoni akaona ya kuwa ni malaika wa BWANA; Gideoni akasema, Ole wangu, Ee Bwana MUNGU! Kwa kuwa nimemwona BWANA uso kwa uso. 23 Dan 10:19;Lk 24:36BWANA akamwambia "Amani iwe pamoja nawe; usiogope; hutakufa". 24 Mwa 22:14;Kut 17:15;Yer 33:16;Eze 48:35;Amu 8:32Ndipo Gideoni akamjengea BWANA madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu;6:24 Yehova-shalomu: maana yake ni, BWANA ni Amani. hata hivi leo iko huko katika Ofra ya Waabiezeri.