11 Malaika wa Mwenyezi Mungu akaja akaketi chini ya mwaloni ulio Ofra, ambao ulikuwa mali ya Yoashi Mwabiezeri, pale Gideoni mwanawe alikuwa akipepeta ngano penye shinikizo la kukamulia zabibu, ili kuificha Wamidiani wasiione. 12 Malaika wa Mwenyezi Mungu alipomtokea Gideoni, akamwambia, "Mwenyezi Mungu yu pamoja nawe, ewe shujaa mwenye nguvu."
22 Gideoni alipotambua kuwa ni malaika wa Mwenyezi Mungu, akapaza sauti, akasema, "Ole wangu, Bwana Mungu Mwenyezi! Kwa kuwa nimemwona malaika wa Mwenyezi Mungu uso kwa uso!"
23 Lakini Mwenyezi Mungu akamwambia, "Amani iwe kwako! Usiogope. Hutakufa."
24 Hivyo Gideoni akamjengea Mwenyezi Mungu madhabahu mahali pale na kupaita Yehova-Shalomu6:24 maana yake Mwenyezi Mungu ni Amani. Hata leo imesimama huko Ofra ya Waabiezeri.