43 Yesu alipokuwa bado anazungumza, Yuda, mmoja wa wale wanafunzi Kumi na Wawili, akatokea. Alikuwa amefuatana na umati wa watu wenye panga na marungu, waliokuwa wametumwa na viongozi wa makuhani, walimu wa sheria, na wazee.
44 Basi msaliti alikuwa amewapa hao watu ishara, kwamba: "Yule nitakayembusu ndiye. Mkamateni, mkamchukue chini ya ulinzi." 45 Mara Yuda akamjia Yesu na kusema, "Rabi."14:45 Rabi ni neno la Kiebrania ambalo maana yake ni daktari, mwalimu au bwana. Walikuwa na madaraja matatu: La chini kabisa Rab (bwana), la pili Rabi (bwana wangu), na la juu kabisa Raboni (mkuu wangu, bwana wangu mkuu). Akambusu. 46 Wale watu wakamkamata Yesu, wakamweka chini ya ulinzi.
50 Ndipo wanafunzi wake wote wakamwacha, wakakimbia.