Kusalitiwa na kukamatwa kwa Yesu
43 Mt 26:47-58;Lk 22:47-55;Yn 18:2-18Basi alipokuwa katika kusema, mara Yuda alifika, mmoja wa wale Kumi na Wawili, na pamoja naye mkutano, wakiwa na panga na marungu, wametoka kwa wakuu wa makuhani, na waandishi, na wazee. 44 Na yule anayemsaliti alikuwa amewapa ishara, akisema, Nitakayembusu, huyo ndiye; mkamateni na kumpeleka chini ya ulinzi. 45 Basi alipokuja, mara akamwendea, akasema, Rabi, akambusu. 46 Wakanyosha mikono yao wakamkamata. 50 Ndipo wakamwacha, wakakimbia wote.