Pular para o conteúdo
Publicidade

Marko 14:43-46,50

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

43 Isa alipokuwa bado anazungumza, Yuda, mmoja wa wale kumi na wawili, akatokea. Alikuwa amefuatana na umati wa watu wenye panga na marungu, waliokuwa wametumwa na viongozi wa makuhani, walimu wa Torati, na wazee.

44 Basi msaliti alikuwa amewapa hao watu ishara, kwamba: "Yule nitakayembusu ndiye. Mkamateni, mkamchukue chini ya ulinzi." 45 Mara Yuda akamjia Isa na kusema, "Mwalimu." Akambusu. 46 Wale watu wakamkamata Isa, wakamweka chini ya ulinzi.

50 Ndipo wanafunzi wake wote wakamwacha, wakakimbia.

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    43 Mt 26:47-58;Lk 22:47-55;Yn 18:2-18Basi alipokuwa katika kusema, mara Yuda alifika, mmoja wa wale Kumi na Wawili, na pamoja naye mkutano, wakiwa na panga na marungu, wametoka kwa wakuu wa makuhani, na waandishi, na wazee. 44 Na yule anayemsaliti alikuwa amewapa ishara, akisema, Nitakayembusu, huyo ndiye; mkamateni na kumpeleka chini ya ulinzi. 45 Basi alipokuja, mara akamwendea, akasema, Rabi, akambusu. 46 Wakanyosha mikono yao wakamkamata. 50 Ndipo wakamwacha, wakakimbia wote.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    43 Yesu alipokuwa bado anazungumza, Yuda, mmoja wa wale wanafunzi Kumi na Wawili, akatokea. Alikuwa amefuatana na umati wa watu wenye panga na marungu, waliokuwa wametumwa na viongozi wa makuhani, walimu wa sheria, na wazee.

    44 Basi msaliti alikuwa amewapa hao watu ishara, kwamba: "Yule nitakayembusu ndiye. Mkamateni, mkamchukue chini ya ulinzi." 45 Mara Yuda akamjia Yesu na kusema, "Rabi."14:45 Rabi ni neno la Kiebrania ambalo maana yake ni daktari, mwalimu au bwana. Walikuwa na madaraja matatu: La chini kabisa Rab (bwana), la pili Rabi (bwana wangu), na la juu kabisa Raboni (mkuu wangu, bwana wangu mkuu). Akambusu. 46 Wale watu wakamkamata Yesu, wakamweka chini ya ulinzi.

    50 Ndipo wanafunzi wake wote wakamwacha, wakakimbia.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.