17 Mtu mmoja miongoni mwa ule umati wa watu akajibu, "Mwalimu, nilimleta kwako mwanangu ambaye ana pepo mchafu anayemfanya asiweze kuongea.
22 Mara kwa mara huyo pepo mchafu amekuwa akimwangusha kwenye moto au kwenye maji ili kumwangamiza. Lakini kama unaweza kufanya jambo lolote, tafadhali tuhurumie utusaidie."
23 Yesu akamwambia, "Kama ukiweza kuamini, yote yawezekana kwake yeye aaminiye."
24 Mara baba yake yule mvulana akapiga kelele akisema, "Ninaamini. Nisaidie kutokuamini kwangu!"