Pular para o conteúdo
Publicidade

Marko 9:17,22-24

SRUV Swahili Revised Union Version

17 Mtu mmoja katika mkutano akamjibu, Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo bubu; 22 Na mara nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno lolote, utuhurumie, na kutusaidia. 23 Mk 11:23Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye. 24 Lk 17:5Mara babaye yule kijana akapaza sauti, akasema, Naamini, nisaidie kutoamini kwangu.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    17 Mtu mmoja miongoni mwa umati ule wa watu akajibu, "Mwalimu, nilimleta kwako mwanangu ambaye ana pepo mchafu anayemfanya asiweze kuongea.

    22 Mara kwa mara huyo pepo mchafu amekuwa akimwangusha kwenye moto au kwenye maji ili kumwangamiza. Lakini kama unaweza kufanya jambo lolote, tafadhali tuhurumie utusaidie."

    23 Isa akamwambia, "Ati, ‘Kama unaweza kufanya jambo lolote’? Yote yawezekana kwake yeye aaminiye."

    24 Mara baba yake yule mvulana akapaza sauti akisema, "Ninaamini. Nisaidie kutokuamini kwangu!"

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    17 Mtu mmoja miongoni mwa ule umati wa watu akajibu, "Mwalimu, nilimleta kwako mwanangu ambaye ana pepo mchafu anayemfanya asiweze kuongea.

    22 Mara kwa mara huyo pepo mchafu amekuwa akimwangusha kwenye moto au kwenye maji ili kumwangamiza. Lakini kama unaweza kufanya jambo lolote, tafadhali tuhurumie utusaidie."

    23 Yesu akamwambia, "Kama ukiweza kuamini, yote yawezekana kwake yeye aaminiye."

    24 Mara baba yake yule mvulana akapiga kelele akisema, "Ninaamini. Nisaidie kutokuamini kwangu!"

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.