17 Mtu mmoja miongoni mwa umati ule wa watu akajibu, "Mwalimu, nilimleta kwako mwanangu ambaye ana pepo mchafu anayemfanya asiweze kuongea.
22 Mara kwa mara huyo pepo mchafu amekuwa akimwangusha kwenye moto au kwenye maji ili kumwangamiza. Lakini kama unaweza kufanya jambo lolote, tafadhali tuhurumie utusaidie."
23 Isa akamwambia, "Ati, ‘Kama unaweza kufanya jambo lolote’? Yote yawezekana kwake yeye aaminiye."
24 Mara baba yake yule mvulana akapaza sauti akisema, "Ninaamini. Nisaidie kutokuamini kwangu!"