Mfano Wa Mtumishi Asiyesamehe
23 "Kwa hiyo Ufalme wa Mbinguni unaweza kufananishwa na mfalme aliyetaka kufanya hesabu zake za fedha na watumishi wake. 24 Alipoanza kufanya hesabu zake, mtu mmoja aliyekuwa anadaiwa talanta18:24 Talanta moja ni sawa na mshahara wa kibarua wa miaka 15. 10,000, aliletwa kwake.
27 Yule bwana wa huyo mtumishi akamwonea huruma, akafuta deni lake lote, akamwacha aende zake.
28 "Lakini yule mtumishi alipokuwa anatoka nje, akakutana na mtumishi mwenzake aliyekuwa amemkopesha dinari 18:28 Dinari moja ilikuwa kama mshahara wa kibarua wa siku moja. mia moja. Akamkamata, akamkaba koo akimwambia, ‘Nilipe kile ninachokudai!’
32 "Yule bwana akamwita yule mtumishi akamwambia, ‘Wewe mtumishi mwovu! Mimi nilikusamehe deni lako lote uliponisihi. 33 Je, haikukupasa kumhurumia mtumishi mwenzako kama mimi nilivyokuhurumia wewe?’