Mfano wa mtumishi asiyesamehe
23 Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake. 24 Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja mwenye deni la talanta18:24 Talanta moja ni kama shilingi 5,000. elfu kumi. 27 Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni. 28 Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa watumishi wake, aliyemwia dinari18:28 Dinari moja ni kama senti 75. mia; akamkamata, akamkaba koo, akisema, Nilipe unachodaiwa. 32 Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nilikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi; 33 nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mtumwa mwenzako, kama mimi nilivyokurehemu wewe?