Pular para o conteúdo
Publicidade

Mathayo 18:23,24,27,28,32,33

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

Mfano wa mtumishi asiyesamehe

23 "Kwa hiyo ufalme wa mbinguni unaweza kufananishwa na mfalme aliyetaka kufanya hesabu zake za fedha na watumishi wake. 24 Alipoanza kufanya hesabu zake, mtu mmoja aliyekuwa anadaiwa talanta18:24 Talanta moja ni sawa na mshahara wa kibarua wa miaka 15. elfu kumi aliletwa kwake.

27 Yule bwana wa huyo mtumishi akamwonea huruma, akafuta deni lake lote, akamwacha aende zake.

28 "Lakini yule mtumishi alipokuwa anatoka nje, akakutana na mtumishi mwenzake aliyekuwa amemkopesha dinari18:28 Dinari moja ilikuwa kama mshahara wa kibarua wa siku moja. mia moja. Akamkamata, akamkaba koo akimwambia, ‘Nilipe kile ninachokudai!’

32 "Yule bwana akamwita yule mtumishi akamwambia, ‘Wewe mtumishi mwovu! Mimi nilikusamehe deni lako lote uliponisihi. 33 Je, haikukupasa kumhurumia mtumishi mwenzako kama mimi nilivyokuhurumia wewe?’

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    23 Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake. 24 Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja mwenye deni la talanta18:24 Talanta moja ni kama shilingi 5,000. elfu kumi. 27 Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni. 28 Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa watumishi wake, aliyemwia dinari18:28 Dinari moja ni kama senti 75. mia; akamkamata, akamkaba koo, akisema, Nilipe unachodaiwa. 32 Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nilikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi; 33 nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mtumwa mwenzako, kama mimi nilivyokurehemu wewe?

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    23 "Kwa hiyo Ufalme wa Mbinguni unaweza kufananishwa na mfalme aliyetaka kufanya hesabu zake za fedha na watumishi wake. 24 Alipoanza kufanya hesabu zake, mtu mmoja aliyekuwa anadaiwa talanta18:24 Talanta moja ni sawa na mshahara wa kibarua wa miaka 15. 10,000, aliletwa kwake.

    27 Yule bwana wa huyo mtumishi akamwonea huruma, akafuta deni lake lote, akamwacha aende zake.

    28 "Lakini yule mtumishi alipokuwa anatoka nje, akakutana na mtumishi mwenzake aliyekuwa amemkopesha dinari 18:28 Dinari moja ilikuwa kama mshahara wa kibarua wa siku moja. mia moja. Akamkamata, akamkaba koo akimwambia, ‘Nilipe kile ninachokudai!’

    32 "Yule bwana akamwita yule mtumishi akamwambia, ‘Wewe mtumishi mwovu! Mimi nilikusamehe deni lako lote uliponisihi. 33 Je, haikukupasa kumhurumia mtumishi mwenzako kama mimi nilivyokuhurumia wewe?’

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.