69 Wakati huu Petro alikuwa amekaa nje uani. Mtumishi mmoja wa kike akamjia na kumwambia, "Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilaya."
70 Lakini Petro akakana mbele yao wote akisema, "Sijui hilo usemalo."
72 Akakana tena kwa kiapo akisema, "Mimi simjui huyo!"
74 Ndipo Petro akaanza kujilaani na kuwaapia, "Mimi simjui mtu huyo!"
Papo hapo jogoo akawika. 75 Ndipo Petro akakumbuka lile neno Yesu alilokuwa amesema: "Kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu." Naye akaenda nje, akalia kwa majonzi.