Pular para o conteúdo
Publicidade

Mathayo 26:69,70,72,74,75

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

69 Wakati huu Petro alikuwa amekaa nje uani. Mjakazi mmoja akamjia na kumwambia, "Wewe pia ulikuwa pamoja na Isa wa Galilaya."

70 Lakini Petro akakana mbele yao wote akisema, "Sijui hilo usemalo."

72 Akakana tena kwa kiapo akisema, "Mimi simjui huyo!"

74 Ndipo Petro akaanza kujilaani na kuwaapia, "Mimi simjui mtu huyo!"

Papo hapo jogoo akawika. 75 Ndipo Petro akakumbuka lile neno Isa alilokuwa amesema: "Kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu." Naye akaenda nje, akalia kwa majonzi.

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    69 Na Petro alikuwa ameketi nje uani; kijakazi mmoja akamwendea, akasema, Wewe nawe ulikuwapo pamoja na Yesu wa Galilaya. 70 Akakana mbele ya wote, akisema, Sijui usemalo. 72 Akakana tena kwa kiapo, Simjui mtu huyu. 74 Ndipo akaanza kulaani na kuapa akisema, Simjui mtu huyu. Na mara jogoo akawika. 75 Mt 26:34Petro akalikumbuka lile neno la Yesu alilolisema, Kabla ya jogoo kuwika, utanikana mara tatu. Akatoka nje, akalia kwa majonzi.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    69 Wakati huu Petro alikuwa amekaa nje uani. Mtumishi mmoja wa kike akamjia na kumwambia, "Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilaya."

    70 Lakini Petro akakana mbele yao wote akisema, "Sijui hilo usemalo."

    72 Akakana tena kwa kiapo akisema, "Mimi simjui huyo!"

    74 Ndipo Petro akaanza kujilaani na kuwaapia, "Mimi simjui mtu huyo!"

    Papo hapo jogoo akawika. 75 Ndipo Petro akakumbuka lile neno Yesu alilokuwa amesema: "Kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu." Naye akaenda nje, akalia kwa majonzi.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.