Petro amkana Yesu
69 Na Petro alikuwa ameketi nje uani; kijakazi mmoja akamwendea, akasema, Wewe nawe ulikuwapo pamoja na Yesu wa Galilaya. 70 Akakana mbele ya wote, akisema, Sijui usemalo. 72 Akakana tena kwa kiapo, Simjui mtu huyu. 74 Ndipo akaanza kulaani na kuapa akisema, Simjui mtu huyu. Na mara jogoo akawika. 75 Mt 26:34Petro akalikumbuka lile neno la Yesu alilolisema, Kabla ya jogoo kuwika, utanikana mara tatu. Akatoka nje, akalia kwa majonzi.