27 Kisha askari wa mtawala wakampeleka Yesu kwenye Praitorio27:27 Praitorio maana yake ni makao makuu ya mtawala, jumba la kifalme lililokuwa linakaliwa na Pontio Pilato huko Yerusalemu, palipokuwa na kiti cha hukumu. na wakakusanya kikosi kizima cha askari kumzunguka. 28 Wakamvua nguo zake na kumvika vazi la rangi nyekundu, kisha 29 wakasokota taji ya miiba, wakaiweka kichwani pake. Wakamwekea fimbo katika mkono wake wa kuume, na wakapiga magoti mbele zake na kumdhihaki, wakisema, "Salamu, mfalme wa Wayahudi!" 30 Wakamtemea mate, wakachukua ile fimbo wakampiga kichwani tena na tena. 31 Baada ya kumdhihaki, wakamvua lile joho, wakamvika tena nguo zake. Kisha wakampeleka ili wakamsulubishe.
Yesu Asulubishwa
(Marko 15:21-32; Luka 23:26-43; Yohana 19:17-27)