Askari wamdhihaki Yesu
27 Mk 15:16-19;Yn 19:2,3Ndipo askari wa mtawala wakamchukua Yesu ndani ya Praitorio,27:27 Praitorio, maana yake ni Nyumba ya Uliwali. wakamkusanyikia kikosi kizima. 28 Wakamvua nguo, wakamvika vazi jekundu. 29 Wakasokota taji la miiba, wakaliweka juu ya kichwa chake, na mwanzi katika mkono wake wa kulia; wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki, wakisema, Salamu, Mfalme wa Wayahudi! 30 Isa 50:6Kisha wakamtemea mate, wakautwaa ule mwanzi, wakampigapiga kichwani. 31 Mk 15:20-41;Lk 23:26,33-49;Yn 19:16-30Walipokwisha kumdhihaki, wakalivua lile vazi, wakamvika mavazi yake, wakamchukua kumsulubisha.