27 Kisha askari wa mtawala wakampeleka Isa kwenye Praitorio27:27 Praitorio ilikuwa makao makuu ya mtawala wa jimbo. Hapa ni jumba la kifalme ambapo Pontio Pilato aliishi huko Yerusalemu, palipokuwa na kiti cha hukumu., na wakakusanya kikosi kizima cha askari kumzunguka. 28 Wakamvua nguo zake na kumvika vazi la rangi nyekundu, kisha 29 wakasokota taji la miiba, wakaiweka kichwani pake. Wakamwekea fimbo katika mkono wake wa kuume, na wakapiga magoti mbele zake na kumdhihaki, wakisema, "Salamu, mfalme wa Wayahudi!" 30 Wakamtemea mate, wakachukua ile fimbo wakampiga kichwani tena na tena. 31 Baada ya kumdhihaki, wakamvua lile joho, wakamvika tena nguo zake. Kisha wakampeleka ili wakamsulubishe.
Isa asulubishwa
(Marko 15:21-32; Luka 23:26-43; Yohana 19:17-27)