Miriamu Na Aroni Wampinga Mose
1 Miriamu na Aroni walianza kuzungumza dhidi ya Mose kwa sababu ya mke wake Mkushi, kwa kuwa alikuwa ameoa Mkushi. 2 Waliuliza, "Je, Bwana amesema kupitia Mose peke yake? Je, hajasema kutupitia sisi pia?" Naye Bwana akasikia hili.
3 (Basi Mose alikuwa mtu mnyenyekevu sana, mnyenyekevu kuliko mtu mwingine yeyote katika uso wa dunia.)
8 Kwake nitanena naye uso kwa uso,
waziwazi wala si kwa mafumbo;
yeye ataona umbo la Bwana.
Kwa nini basi ninyi hamkuogopa
kuzungumza kinyume cha mtumishi wangu Mose?"