Miriamu na Haruni wampinga Musa
1 Miriamu na Haruni walianza kuzungumza dhidi ya Musa kwa sababu ya mke wake Mkushi, kwa kuwa alikuwa ameoa Mkushi. 2 Waliuliza, "Je, Mwenyezi Mungu amesema kupitia Musa peke yake? Je, hajasema kutupitia sisi pia?" Naye Mwenyezi Mungu akasikia hili.
3 (Basi Musa alikuwa mtu mnyenyekevu sana, mnyenyekevu kuliko mtu mwingine yeyote katika uso wa dunia.)
8 Kwake nitanena naye uso kwa uso,
waziwazi wala si kwa mafumbo;
yeye ataona umbo la Mwenyezi Mungu.
Kwa nini basi ninyi hamkuogopa
kuzungumza kinyume cha mtumishi wangu Musa?"