Pular para o conteúdo
Publicidade

Ruthu 2:2,3,10-12

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

2 Ruthu, Mmoabu, akamwambia Naomi, "Nitakwenda mashambani nikaokote mabaki ya nafaka nyuma ya yule nitakayepata kibali machoni pake."

Naomi akamwambia, "Nenda, binti yangu." 3 Basi akaenda, akaokota mabaki ya nafaka mashambani nyuma ya wavunaji. Ikatokea kwamba alijikuta anafanya kazi kwenye shamba lililokuwa mali ya Boazi, ambaye alitoka kwenye ukoo wa Elimeleki.

10 Kwa ajili ya hili, akasujudu mpaka nchi, akamwambia, "Jinsi gani nimepata kibali machoni pako, hata ukanijali mimi mgeni?"

11 Boazi akamjibu, "Nimeambiwa yote uliyomtendea mama mkwe wako tangu mume wako alipofariki, na jinsi ulivyomwacha baba yako na mama yako na nchi yako ulimozaliwa, ukaja kuishi na watu ambao hukuwafahamu awali. 12 Bwana na akulipe kwa yale uliyoyatenda. Ubarikiwe kwa wingi na Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye umekimbilia mabawani mwake."

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    2 Ruthu, Mmoabu, akamwambia Naomi, "Nitaenda mashambani nikaokote mabaki ya nafaka nyuma ya yule nitakayepata kibali machoni pake."

    Naomi akamwambia, "Nenda, binti yangu." 3 Basi akaenda, akaokota mabaki ya nafaka mashambani nyuma ya wavunaji. Ikatokea kwamba alijikuta akifanya kazi kwenye shamba lililokuwa mali ya Boazi, ambaye alikuwa wa ukoo wa Elimeleki.

    10 Aliposikia hili, akasujudu, uso wake ukagusa chini, akamwambia, "Jinsi gani nimepata kibali machoni pako, hata ukanijali mimi mgeni?"

    11 Boazi akamjibu, "Nimeambiwa yote uliyomtendea mama mkwe wako tangu mume wako alipofariki, na jinsi ulivyomwacha baba yako na mama yako na nchi yako ulimozaliwa, ukaja kuishi na watu ambao hukuwafahamu awali. 12 Mwenyezi Mungu na akulipe kwa yale uliyoyatenda. Ubarikiwe kwa wingi na Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, ambaye umekimbilia mabawani mwake."

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    2 Law 19:9-10;23:22;Kum 24:19Naye Ruthu Mmoabi akamwambia Naomi, Niruhusu niende shambani, niokote mabaki ya masuke nyuma yake yule ambaye nitaona kibali machoni pake. Akamwambia, Haya, mwanangu, nenda. 3 Basi akaenda, akaja akaokota mabaki shambani nyuma ya wavunaji; na kwa bahati akafikia sehemu ya shamba la Boazi, ambaye alikuwa wa jamaa yake Elimeleki.

    10 Mwa 18:2;1 Sam 25:23Ndipo aliposujudia, akainama mpaka nchi, akamwambia, Jinsi gani nimepata kibali machoni pako, hata ukanifahamu, mimi niliye mgeni? 11 Mit 31:31;Rut 1:14;Lk 5:11,28;14:33;18:29,30;Ebr 11:8,9,24-26Naye Boazi akajibu, akamwambia, Nimeelezwa sana yote uliyomfanyia mkweo, tangu alipokufa mumeo; na jinsi ulivyowaacha baba yako na mama yako, na nchi yako uliyozaliwa, ukawafikia watu usiowajua tangu hapo. 12 1 Sam 24:19;Zab 19:11;58:11;Mit 11:18;Mt 5:12;6:1;Lk 6:35;14:12-14;2 Tim 1:18;Ebr 6:10;11:6,26;Zab 17:8;36:7BWANA akujaze kwa kazi yako, nawe upewe thawabu kamili na BWANA, Mungu wa Israeli, ambaye umekuja kukimbilia chini ya mabawa yake.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Rute
Ver todos os capítulos de Rute