2 Ruthu, Mmoabu, akamwambia Naomi, "Nitaenda mashambani nikaokote mabaki ya nafaka nyuma ya yule nitakayepata kibali machoni pake."
Naomi akamwambia, "Nenda, binti yangu." 3 Basi akaenda, akaokota mabaki ya nafaka mashambani nyuma ya wavunaji. Ikatokea kwamba alijikuta akifanya kazi kwenye shamba lililokuwa mali ya Boazi, ambaye alikuwa wa ukoo wa Elimeleki.
10 Aliposikia hili, akasujudu, uso wake ukagusa chini, akamwambia, "Jinsi gani nimepata kibali machoni pako, hata ukanijali mimi mgeni?"
11 Boazi akamjibu, "Nimeambiwa yote uliyomtendea mama mkwe wako tangu mume wako alipofariki, na jinsi ulivyomwacha baba yako na mama yako na nchi yako ulimozaliwa, ukaja kuishi na watu ambao hukuwafahamu awali. 12 Mwenyezi Mungu na akulipe kwa yale uliyoyatenda. Ubarikiwe kwa wingi na Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, ambaye umekimbilia mabawani mwake."