2 Law 19:9-10;23:22;Kum 24:19Naye Ruthu Mmoabi akamwambia Naomi, Niruhusu niende shambani, niokote mabaki ya masuke nyuma yake yule ambaye nitaona kibali machoni pake. Akamwambia, Haya, mwanangu, nenda. 3 Basi akaenda, akaja akaokota mabaki shambani nyuma ya wavunaji; na kwa bahati akafikia sehemu ya shamba la Boazi, ambaye alikuwa wa jamaa yake Elimeleki.
10 Mwa 18:2;1 Sam 25:23Ndipo aliposujudia, akainama mpaka nchi, akamwambia, Jinsi gani nimepata kibali machoni pako, hata ukanifahamu, mimi niliye mgeni? 11 Mit 31:31;Rut 1:14;Lk 5:11,28;14:33;18:29,30;Ebr 11:8,9,24-26Naye Boazi akajibu, akamwambia, Nimeelezwa sana yote uliyomfanyia mkweo, tangu alipokufa mumeo; na jinsi ulivyowaacha baba yako na mama yako, na nchi yako uliyozaliwa, ukawafikia watu usiowajua tangu hapo. 12 1 Sam 24:19;Zab 19:11;58:11;Mit 11:18;Mt 5:12;6:1;Lk 6:35;14:12-14;2 Tim 1:18;Ebr 6:10;11:6,26;Zab 17:8;36:7BWANA akujaze kwa kazi yako, nawe upewe thawabu kamili na BWANA, Mungu wa Israeli, ambaye umekuja kukimbilia chini ya mabawa yake.