Pular para o conteúdo
Publicidade

Yakobo 4:13-17

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

Kujivuna Kwa Ajili Ya Kesho

13 Basi sikilizeni ninyi msemao, "Leo au kesho tutakwenda katika mji huu ama ule tukae humo mwaka mmoja, tufanye biashara na kupata faida." 14 Lakini hamjui hata litakalotukia kesho. Maisha yenu ni nini? Ninyi ni ukungu ambao huonekana kwa kitambo kidogo kisha hutoweka. 15 Badala yake, inawapasa kusema, "Kama Bwana akipenda, tutaishi na kufanya hili ama lile." 16 Kama ilivyo sasa, mnajisifu na kujigamba. Kujisifu kwa namna hiyo ni uovu. 17 Basi mtu yeyote anayejua jema limpasalo kutenda, lakini asilitende, mtu huyo anatenda dhambi.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    13 Basi sikilizeni ninyi msemao, "Leo au kesho tutaenda katika mji huu ama ule tukae humo mwaka mmoja, tufanye biashara na kupata faida." 14 Lakini hamjui hata litakalotukia kesho. Maisha yenu ni nini? Ninyi ni ukungu ambao huonekana kwa kitambo kidogo kisha hutoweka. 15 Badala yake, inawapasa kusema, "Kama Mwenyezi Mungu akipenda, tutaishi na kufanya hili ama lile." 16 Ilivyo sasa, mnajisifu na kujigamba. Kujisifu kote kwa namna hii ni uovu. 17 Basi mtu yeyote anayejua jema limpasalo kutenda, lakini asilitende, mtu huyo anatenda dhambi.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    13 Mit 27:1Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida; 14 Lk 12:20;Zab 39:5,11lakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa muda mfupi tu, kisha hutoweka. 15 Mdo 18:21Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi. 16 Lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu; kujisifu kote kwa namna hii ni kubaya. 17 Lk 12:47;Rum 14:23Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.