Pular para o conteúdo
Publicidade

Yakobo 4:6-10

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

6 Lakini yeye hutupatia neema zaidi. Hii ndiyo sababu Andiko husema:

"Mungu huwapinga wenye kiburi,

lakini huwapa wanyenyekevu neema."

7 Basi mtiini Mungu. Mpingeni ibilisi, naye atawakimbia. 8 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu ninyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu ninyi wenye nia mbili. 9 Huzunikeni, ombolezeni na kulia. Kicheko chenu na kigeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa huzuni. 10 Jinyenyekezeni mbele za Bwana, naye atawainua.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    6 Lakini yeye hutupatia neema zaidi. Hii ndiyo sababu Maandiko yasema:

    "Mungu huwapinga wenye kiburi,

    lakini huwapa wanyenyekevu neema."

    7 Basi mtiini Mungu. Mpingeni ibilisi, naye atawakimbia. 8 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia. Itakaseni mikono yenu ninyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu ninyi wenye nia mbili. 9 Huzunikeni, na mwomboleze, na kulia. Kicheko chenu na kigeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa huzuni. 10 Jinyenyekezeni mbele za Mwenyezi Mungu, naye atawainua.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    6 Mit 3:34;Ayu 22:29;Mt 23:12;1 Pet 5:5Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu. 7 Efe 6:12;1 Pet 5:8,9Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. 8 Zek 1:3;Isa 1:16Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. 9 Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa huzuni kubwa. 10 1 Pet 5:6Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.